Kumbukumbu 32:6
Deuteronomy 32:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, hii ndiyo njia ya kumlipa Bwana, enyi watu wajinga na wasio na busara? Je, yeye siye Baba yenu, Muumba wenu, aliyewafanya ninyi na kuwaumba?
Deuteronomy 32:6 in English
Deuteronomy 32:6 · Berean Standard Bible
Is this how you repay the LORD, O foolish and senseless people? Is He not your Father and Creator? Has He not made you and established you?
Context
4Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu,
njia zake zote ni haki.
Mungu mwaminifu ambaye hakosei,
yeye ni mnyofu na mwenye haki. 5Wamefanya mambo ya upotovu mbele zake;
kwa aibu yao, wao si watoto wake tena,
lakini ni kizazi kilicho kiovu na kilichopotoka. 6Je, hii ndiyo njia ya kumlipa Bwana,
enyi watu wajinga na wasio na busara?
Je, yeye siye Baba yenu, Muumba wenu,
aliyewafanya ninyi na kuwaumba? 7Kumbuka siku za kale;
tafakari vizazi vya zamani vilivyopita.
Uliza baba yako, naye atakuambia,
wazee wako, nao watakueleza. 8Aliye Juu Sana alipowapa mataifa urithi wao,
alipogawanya wanadamu wote,
aliweka mipaka kwa ajili ya mataifa
sawasawa na hesabu ya wana wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.