Kumbukumbu 32:40
Deuteronomy 32:40 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema: Hakika kama niishivyo milele,
Deuteronomy 32:40 in English
Deuteronomy 32:40 · Berean Standard Bible
For I lift up My hand to heaven and declare: As surely as I live forever,
Context
38miungu wale waliokula mafuta ya dhabihu zao
na kunywa mvinyo wa sadaka zao za vinywaji?
Wainuke basi, wawasaidie!
Wawapeni basi ulinzi! 39“Tazama basi, Mimi mwenyewe, Mimi Ndiye!
Hakuna mungu mwingine ila Mimi.
Mimi ninaua na Mimi ninafufua,
Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya,
wala hakuna awezaye kuokoa kutoka mkononi mwangu. 40Ninainua mkono wangu kuelekea mbinguni na kusema:
Hakika kama niishivyo milele, 41wakati ninapounoa upanga wangu unaometameta
na mkono wangu unapoushika ili kutoa hukumu,
nitalipiza kisasi juu ya adui zangu
na kuwalipiza wale wanaonichukia. 42Nitailevya mishale yangu kwa damu,
wakati upanga wangu ukitafuna nyama:
damu ya waliochinjwa pamoja na mateka,
vichwa vya viongozi wa adui.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.