Kumbukumbu 32:3
Deuteronomy 32:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitalitangaza jina la Bwana. Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu!
Deuteronomy 32:3 in English
Deuteronomy 32:3 · Berean Standard Bible
For I will proclaim the name of the LORD. Ascribe greatness to our God!
Context
1Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema;
sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu. 2Mafundisho yangu na yanyeshe kama mvua,
na maneno yangu na yashuke kama umande,
kama manyunyu juu ya majani mabichi,
kama mvua tele juu ya mimea myororo. 3Nitalitangaza jina la Bwana.
Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! 4Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu,
njia zake zote ni haki.
Mungu mwaminifu ambaye hakosei,
yeye ni mnyofu na mwenye haki. 5Wamefanya mambo ya upotovu mbele zake;
kwa aibu yao, wao si watoto wake tena,
lakini ni kizazi kilicho kiovu na kilichopotoka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.