Kumbukumbu 32:23
Deuteronomy 32:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nitalundika majanga juu yao na kutumia mishale yangu dhidi yao.
Deuteronomy 32:23 in English
Deuteronomy 32:23 · Berean Standard Bible
I will heap disasters upon them; I will spend My arrows against them.
Context
21Wamenifanya niwe na wivu
kwa kile ambacho si mungu,
na kunikasirisha kwa sanamu zao
zisizokuwa na thamani.
Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa.
Nitawafanya wakasirishwe
na taifa lile lisilo na ufahamu. 22Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu,
ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti.
Utateketeza dunia pamoja na mazao yake,
na kuwasha moto katika misingi ya milima. 23“Nitalundika majanga juu yao
na kutumia mishale yangu dhidi yao. 24Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya,
yateketezayo na tauni ya kufisha;
nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu,
na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini. 25Barabarani upanga utawakosesha watoto;
nyumbani mwao hofu itatawala.
Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia,
pia watoto wachanga na wazee wenye mvi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.