Kumbukumbu 32:20
Deuteronomy 32:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akasema, “Nitawaficha uso wangu, nami nione mwisho wao utakuwa nini, kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka, watoto ambao si waaminifu.
Deuteronomy 32:20 in English
Deuteronomy 32:20 · Berean Standard Bible
He said: “I will hide My face from them; I will see what will be their end. For they are a perverse generation— children of unfaithfulness.
Context
18Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi;
mkamsahau Mungu aliyewazaa. 19Bwana akaona hili, akawakataa,
kwa sababu alikasirishwa
na wanawe na binti zake. 20Akasema, “Nitawaficha uso wangu,
nami nione mwisho wao utakuwa nini,
kwa kuwa wao ni kizazi kilichopotoka,
watoto ambao si waaminifu. 21Wamenifanya niwe na wivu
kwa kile ambacho si mungu,
na kunikasirisha kwa sanamu zao
zisizokuwa na thamani.
Nitawafanya wawaonee wivu wale ambao si taifa.
Nitawafanya wakasirishwe
na taifa lile lisilo na ufahamu. 22Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu,
ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti.
Utateketeza dunia pamoja na mazao yake,
na kuwasha moto katika misingi ya milima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.