Kumbukumbu 30:8
Deuteronomy 30:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utamtii tena Bwana na kuzishika amri zake zote ninazokupa leo.
Deuteronomy 30:8 in English
Deuteronomy 30:8 · Berean Standard Bible
And you will again obey the voice of the LORD and follow all His commandments I am giving you today.
Context
6Bwana Mungu wako ataitahiri mioyo yenu na mioyo ya wazao wenu ili mweze kumpenda kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote ukaishi. 7Bwana Mungu wako ataweka laana hizi zote juu ya adui zako ambao wanakuchukia na kukutesa. 8Utamtii tena Bwana na kuzishika amri zake zote ninazokupa leo. 9Ndipo Bwana Mungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako. Bwana atakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako, 10kama ukimtii Bwana Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.