Kumbukumbu 3:28
Deuteronomy 3:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ngʼambo na kuwarithisha nchi utakayoiona.”
Deuteronomy 3:28 in English
Deuteronomy 3:28 · Berean Standard Bible
But commission Joshua, encourage him, and strengthen him, for he will cross over ahead of the people and enable them to inherit the land that you will see.”
Context
26Lakini kwa sababu yenu Bwana alinikasirikia na hakutaka kunisikiliza. Bwana aliniambia, “Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena. 27Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie magharibi, kaskazini, kusini na mashariki. Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile wewe hutavuka Yordani. 28Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ngʼambo na kuwarithisha nchi utakayoiona.” 29Kwa hiyo tulikaa kwenye bonde karibu na Beth-Peori.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.