Native Bible

Deuteronomy 3:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huo nilimsihi Bwana:

Deuteronomy 3:23 in English

Deuteronomy 3:23 · Berean Standard Bible

At that time I also pleaded with the LORD:

Context

21Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo Bwana Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. Bwana atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo. 22Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.” 23Wakati huo nilimsihi Bwana: 24“Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe? 25Acha niende nikaione hiyo nchi nzuri ngʼambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.