Kumbukumbu 3:22
Deuteronomy 3:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”
Deuteronomy 3:22 in English
Deuteronomy 3:22 · Berean Standard Bible
Do not be afraid of them, for the LORD your God Himself will fight for you.”
Context
20mpaka hapo Bwana atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, ngʼambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.” 21Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo Bwana Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. Bwana atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo. 22Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.” 23Wakati huo nilimsihi Bwana: 24“Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.