Kumbukumbu 28:24
Deuteronomy 28:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana atafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie.
Deuteronomy 28:24 in English
Deuteronomy 28:24 · Berean Standard Bible
The LORD will turn the rain of your land into dust and powder; it will descend on you from the sky until you are destroyed.
Context
22Bwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie. 23Anga juu yako itakuwa shaba, na ardhi chini yako itakuwa chuma. 24Bwana atafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie. 25Bwana atakufanya ushindwe mbele ya adui zako. Utawajia kwa njia moja lakini utawakimbia mbele yao kwa njia saba, nawe utakuwa kitu cha kuchukiza kwa falme zote za dunia. 26Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu yeyote wa kuwafukuza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.