Kumbukumbu 28:22
Deuteronomy 28:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie.
Deuteronomy 28:22 in English
Deuteronomy 28:22 · Berean Standard Bible
The LORD will strike you with wasting disease, with fever and inflammation, with scorching heat and drought,* and with blight and mildew; these will pursue you until you perish.
Context
20Bwana ataleta laana juu yako, fadhaa na kukaripiwa katika kila kitu unachokigusa kwa mkono wako, mpaka uwe umeharibiwa na kuangamizwa ghafula kwa ajili ya maovu uliyoyafanya kwa kumwacha yeye. 21Bwana atakupiga kwa magonjwa mpaka akuangamize kutoka nchi unayoingia kuimiliki. 22Bwana atakupiga kwa magonjwa ya kudhoofisha, kwa homa na kuwashwa, hari na kwa ukame, kutu na kuwa na uchungu ambavyo vitakupiga mpaka uangamie. 23Anga juu yako itakuwa shaba, na ardhi chini yako itakuwa chuma. 24Bwana atafanya mvua ya nchi yako kuwa mavumbi na mchanga; vitakujia kutoka angani mpaka uangamie.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.