Kumbukumbu 20:9
Deuteronomy 20:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.
Deuteronomy 20:9 in English
Deuteronomy 20:9 · Berean Standard Bible
When the officers have finished addressing the army, they are to appoint commanders to lead it.
Context
7Je, kuna yeyote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.” 8Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.” 9Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi. 10Wakati mtakapokwenda kushambulia mji, wapeni watu wake masharti ya amani. 11Wakikubali na kuwafungulia malango yao, watu wake wote watawatumikia kwa kufanya kazi ngumu na watawatumikia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.