Kumbukumbu 14:19
Deuteronomy 14:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.
Deuteronomy 14:19 in English
Deuteronomy 14:19 · Berean Standard Bible
All flying insects are unclean for you; they may not be eaten.
Context
17mwari, nderi, mnandi, 18korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo. 19Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale. 20Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula. 21Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa Bwana Mungu wenu.
Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.