Native Bible

Deuteronomy 11:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

baraka kama mtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu, ambayo ninawapa leo;

Deuteronomy 11:27 in English

Deuteronomy 11:27 · Berean Standard Bible

a blessing if you obey the commandments of the LORD your God that I am giving you today,

Context

25Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. Bwana Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mwendako. 26Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana: 27baraka kama mtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu, ambayo ninawapa leo; 28laana kama hamtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua. 29Wakati Bwana Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.