Kumbukumbu 11:15
Deuteronomy 11:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.
Deuteronomy 11:15 in English
Deuteronomy 11:15 · Berean Standard Bible
And I will provide grass in the fields for your livestock, and you will eat and be satisfied.
Context
13Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda Bwana Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, 14ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta. 15Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba. 16Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia. 17Ndipo hasira ya Bwana itawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu ili mvua isinyeshe nayo ardhi haitatoa mazao, nanyi mtaangamia mara katika nchi nzuri ambayo Bwana anawapa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.