Native Bible

Deuteronomy 11:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta.

Deuteronomy 11:14 in English

Deuteronomy 11:14 · Berean Standard Bible

then I will provide * rain for your land in season, the autumn and spring rains, that you may gather your grain, new wine, and oil.

Context

12Ni nchi ambayo Bwana Mungu wenu anaitunza; macho ya Bwana Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. 13Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda Bwana Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, 14ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta. 15Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba. 16Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.