Kumbukumbu 1:34
Deuteronomy 1:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati Bwana aliposikia lile mlilosema, alikasirika, akaapa, akasema:
Deuteronomy 1:34 in English
Deuteronomy 1:34 · Berean Standard Bible
When the LORD heard your words, He grew angry and swore an oath, saying,
Context
32Pamoja na hili, hamkumtegemea Bwana Mungu wenu, 33ambaye aliwatangulia katika safari yenu, kwa moto usiku na kwa wingu mchana, kuwatafutia mahali penu pa kupiga kambi na kuwaonyesha njia mtakayoiendea. 34Wakati Bwana aliposikia lile mlilosema, alikasirika, akaapa, akasema: 35“Hakuna mtu wa kizazi hiki kiovu atakayeona nchi nzuri niliyoapa kuwapa baba zenu, 36isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune. Yeye ataiona, nami nitampa yeye na wazao wake nchi aliyoikanyaga kwa miguu, kwa sababu alimfuata Bwana kwa moyo wote.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.