Danieli 3:9
Daniel 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele!
Daniel 3:9 in English
Daniel 3:9 · Berean Standard Bible
saying to King Nebuchadnezzar, “O king, may you live forever!
Context
7Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda na aina zote za ala za uimbaji, watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. 8Wakati huo baadhi ya Wakaldayo walijitokeza na kuwashtaki Wayahudi. 9Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele! 10Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda, zumari na aina zote za ala za uimbaji lazima aanguke chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu, 11na kwamba yeyote ambaye hataanguka chini na kuiabudu atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.