Native Bible

Daniel 3:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huo baadhi ya Wakaldayo walijitokeza na kuwashtaki Wayahudi.

Daniel 3:8 in English

Daniel 3:8 · Berean Standard Bible

At this time some astrologers * came forward and maliciously accused the Jews,

Context

6Mtu yeyote ambaye hataanguka chini na kuiabudu sanamu hiyo, atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.” 7Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda na aina zote za ala za uimbaji, watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha. 8Wakati huo baadhi ya Wakaldayo walijitokeza na kuwashtaki Wayahudi. 9Wakamwambia Mfalme Nebukadneza, “Ee mfalme, uishi milele! 10Ee mfalme, umetoa amri kwamba kila mmoja atakayesikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda, zumari na aina zote za ala za uimbaji lazima aanguke chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.