Danieli 11:43
Daniel 11:43 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibia na Wakushi kwa kujisalimisha.
Daniel 11:43 in English
Daniel 11:43 · Berean Standard Bible
He will gain control of the treasures of gold and silver and over all the riches of Egypt, and the Libyans and Cushites * will also submit to him.
Context
41Pia ataivamia Nchi ya Kupendeza. Nchi nyingi zitapinduliwa, bali Edomu, Moabu na viongozi wa Amoni wataokolewa kutoka mkono wake. 42Atapanua mamlaka yake juu ya nchi nyingi; hata Misri haitaepuka. 43Atamiliki hazina za dhahabu, fedha na utajiri wote wa Misri, pamoja na Walibia na Wakushi kwa kujisalimisha. 44Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamshtua, naye ataondoka kwa ghadhabu nyingi ili kuangamiza na kuharibu kabisa wengi. 45Atasimika hema zake za ufalme kati ya bahari na mlima mtakatifu wa kupendeza. Hata hivyo, atafikia mwisho wake, wala hakuna yeyote atakayemsaidia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.