Wakolosai 3:17
Colossians 3:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye.
Colossians 3:17 in English
Colossians 3:17 · Berean Standard Bible
And whatever you do, in word or deed, do it all in the name of the Lord Jesus, giving thanks to God the Father through Him.
Context
15Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani. 16Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu. 17Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika yeye. 18Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana. 19Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe na uchungu dhidi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.