Amosi 8:9
Amos 8:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Katika siku ile,” asema Bwana Mwenyezi, “Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia iwe giza wakati wa mchana mwangavu.
Amos 8:9 in English
Amos 8:9 · Berean Standard Bible
And in that day, declares the Lord GOD, I will make the sun go down at noon, and I will darken the earth in the daytime.
Context
7Bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya. 8“Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hili,
nao wote waishio ndani mwake hawataomboleza?
Nchi yote itainuka kama Naili;
itapanda na kushuka kama mto wa Misri. 9“Katika siku ile,” asema Bwana Mwenyezi,
“Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia
iwe giza wakati wa mchana mwangavu. 10Nitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo,
na kuimba kwenu kote kuwe kilio.
Nitawafanya ninyi nyote mvae nguo ya gunia
na kunyoa nywele zenu.
Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee,
na mwisho wake kama siku ya uchungu. 11“Siku zinakuja,” asema Bwana Mwenyezi,
“wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote:
si njaa ya chakula wala kiu ya maji,
lakini njaa ya kusikia maneno ya Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.