Amosi 8:6
Amos 8:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
mkiwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu, na mkiuza hata takataka za ngano pamoja na ngano.
Amos 8:6 in English
Amos 8:6 · Berean Standard Bible
Let us buy the poor with silver and the needy for a pair of sandals, selling even the chaff with the wheat!”
Context
4Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji,
na kuwaonea maskini wa nchi, 5mkisema,
“Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita
ili tupate kuuza nafaka,
na Sabato itakwisha lini
ili tuweze kuuza ngano?”
Mkipunguza vipimo,
na kuongeza bei,
na kudanganya kwa mizani zisizo sawa, 6mkiwanunua maskini kwa fedha,
na wahitaji kwa jozi ya viatu,
na mkiuza hata takataka za ngano
pamoja na ngano. 7Bwana ameapa kwake mwenyewe, aliye Kiburi cha Yakobo: “Kamwe sitasahau chochote ambacho wamefanya. 8“Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hili,
nao wote waishio ndani mwake hawataomboleza?
Nchi yote itainuka kama Naili;
itapanda na kushuka kama mto wa Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.