Amosi 8:4
Amos 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji, na kuwaonea maskini wa nchi,
Amos 8:4 in English
Amos 8:4 · Berean Standard Bible
Hear this, you who trample the needy, who do away with the poor of the land,
Context
2Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?”
Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.”
Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.” 3Bwana Mwenyezi asema, “Katika siku ile, nyimbo katika Hekalu zitageuka kuwa maombolezo. Miili mingi, mingi sana: itatupwa kila mahali! Kimya!” 4Lisikieni hili, ninyi ambao mnawagandamiza wahitaji,
na kuwaonea maskini wa nchi, 5mkisema,
“Ni lini Mwezi Mwandamo utakapopita
ili tupate kuuza nafaka,
na Sabato itakwisha lini
ili tuweze kuuza ngano?”
Mkipunguza vipimo,
na kuongeza bei,
na kudanganya kwa mizani zisizo sawa, 6mkiwanunua maskini kwa fedha,
na wahitaji kwa jozi ya viatu,
na mkiuza hata takataka za ngano
pamoja na ngano.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.