Amosi 5:24
Amos 5:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!
Amos 5:24 in English
Amos 5:24 · Berean Standard Bible
But let justice roll on like a river, and righteousness like an ever-flowing stream.
Context
22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka,
sitazikubali.
Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani,
sitazitambua. 23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu!
Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu. 24Lakini acheni haki itiririke kama mto,
na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka! 25“Je, mliniletea dhabihu na sadaka
kwa miaka arobaini kule jangwani,
ee nyumba ya Israeli? 26Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu,
Sikuthi mungu wenu mtawala,
na Kiuni mungu wenu wa nyota,
ambao mliwatengeneza wenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.