Amosi 4:7
Amos 4:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu kabla ya kufikia mavuno. Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja, lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine. Shamba moja lilipata mvua, na lingine halikupata, nalo likakauka.
Amos 4:7 in English
Amos 4:7 · Berean Standard Bible
“I also withheld the rain from you when the harvest was three months away. I sent rain on one city but withheld it from another. One field received rain; another without rain withered.
Context
5Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani,
jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari:
jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli,
kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,”
asema Bwana Mwenyezi. 6“Niliwapa njaa kwenye kila mji,
na ukosefu wa chakula katika kila mji,
hata hivyo bado hamjanirudia mimi,”
asema Bwana. 7“Pia niliwazuilia ninyi mvua miezi mitatu
kabla ya kufikia mavuno.
Nilinyesha mvua kwenye mji mmoja,
lakini niliizuia mvua isinyeshe mji mwingine.
Shamba moja lilipata mvua,
na lingine halikupata, nalo likakauka. 8Watu walitangatanga mji hata mji kutafuta maji,
lakini hawakupata ya kuwatosha kunywa,
hata hivyo hamjanirudia mimi,”
asema Bwana. 9“Mara nyingi nilizipiga bustani zenu na mashamba ya mizabibu,
niliyapiga kwa kutu na ukungu.
Nzige walitafuna tini zenu na miti ya mizeituni,
hata hivyo hamjanirudia mimi,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.