Amosi 3:4
Amos 3:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, simba hunguruma katika kichaka wakati hana mawindo? Aweza kuvuma katika pango wakati ambao hajakamata chochote?
Amos 3:4 in English
Amos 3:4 · Berean Standard Bible
Does a lion roar in the forest when he has no prey? Does a young lion growl in his den if he has caught nothing?
Context
2“Ni ninyi tu niliowachagua
kati ya jamaa zote za dunia;
kwa hiyo nitawaadhibu
kwa ajili ya dhambi zenu zote.” 3Je, watu wawili hutembea pamoja
wasipokubaliana kufanya hivyo? 4Je, simba hunguruma katika kichaka
wakati hana mawindo?
Aweza kuvuma katika pango
wakati ambao hajakamata chochote? 5Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini
ambapo hajategewa chambo?
Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini
wakati ambapo hakuna chochote cha kunasa? 6Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,
watu hawatetemeki?
Mji upatwapo na maafa,
je, si Bwana amesababisha?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.