Amosi 3:14
Amos 3:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake, nitaharibu madhabahu za Betheli; pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali na kuanguka chini.
Amos 3:14 in English
Amos 3:14 · Berean Standard Bible
On the day I punish Israel for their transgressions, I will visit destruction on the altars of Bethel; the horns of the altar will be cut off, and they will fall to the ground.
Context
12Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba
vipande viwili tu vya mfupa wa mguu
au kipande cha sikio,
hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,
wale wakaao Samaria
kwenye kingo za vitanda vyao,
na katika Dameski
kwenye viti vyao vya fahari.” 13“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. 14“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake,
nitaharibu madhabahu za Betheli;
pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali
na kuanguka chini. 15Nitabomoa nyumba ya wakati wa masika,
pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;
nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu
na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.