Amosi 3:11
Amos 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Adui ataizingira nchi; ataangusha chini ngome zenu na kuteka nyara maboma yenu.”
Amos 3:11 in English
Amos 3:11 · Berean Standard Bible
Therefore this is what the Lord GOD says: “An enemy * will surround the land; he will pull down your strongholds and plunder your citadels.”
Context
9Tangazeni katika ngome za Ashdodi
na katika ngome za Misri:
“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;
angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,
na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.” 10Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema,
wale ambao hujilundikia nyara
na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.” 11Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:
“Adui ataizingira nchi;
ataangusha chini ngome zenu
na kuteka nyara maboma yenu.” 12Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba
vipande viwili tu vya mfupa wa mguu
au kipande cha sikio,
hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,
wale wakaao Samaria
kwenye kingo za vitanda vyao,
na katika Dameski
kwenye viti vyao vya fahari.” 13“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.