Native Bible

Amos 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

nitatuma moto juu ya kuta za Gaza ambao utateketeza ngome zake.

Amos 1:7 in English

Amos 1:7 · Berean Standard Bible

So I will send fire upon the walls of Gaza, to consume its citadels.

Context

5Nitalivunja lango la Dameski; nitamwangamiza mfalme aliyeko katika Bonde la Aveni,* na yeye ambaye anaishika fimbo ya utawala katika Beth-Edeni. Watu wote wa Aramu watakwenda uhamishoni huko Kiri,” asema Bwana. 6Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Gaza, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu walichukua mateka jumuiya nzima na kuwauza kwa Edomu, 7nitatuma moto juu ya kuta za Gaza ambao utateketeza ngome zake. 8Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni. Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,” asema Bwana Mwenyezi. 9Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Tiro, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu, na kutokujali mapatano ya undugu,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.