Matendo 9:41
Acts 9:41 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Petro akamshika mkono akamwinua, ndipo akawaita wale watakatifu na wajane akamkabidhi kwao akiwa hai.
Acts 9:41 in English
Acts 9:41 · Berean Standard Bible
Peter took her by the hand and helped her up. Then he called the saints and widows and presented her to them alive.
Context
39Kwa hiyo Petro akainuka akaenda nao, naye alipowasili, wakampeleka hadi kwenye chumba cha ghorofani alipokuwa amelazwa. Wajane wengi walisimama karibu naye wakilia na kuonyesha majoho na nguo nyingine ambazo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa pamoja nao. 40Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi. 41Petro akamshika mkono akamwinua, ndipo akawaita wale watakatifu na wajane akamkabidhi kwao akiwa hai. 42Habari hizi zikajulikana sehemu zote za Yafa na watu wengi wakamwamini Bwana. 43Petro akakaa Yafa kwa siku nyingi akiishi na Simoni mtengenezaji ngozi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.