Matendo 8:33
Acts 8:33 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake. Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake? Kwa maana maisha yake yaliondolewa kutoka duniani.”
Acts 8:33 in English
Acts 8:33 · Berean Standard Bible
In His humiliation He was deprived of justice. Who can recount His descendants? For His life was removed from the earth.”*
Context
31Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye. 32Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko:
“Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni,
kama mwana-kondoo anyamazavyo
mbele yake yule amkataye manyoya,
hivyo hakufungua kinywa chake. 33Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake.
Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake?
Kwa maana maisha yake yaliondolewa
kutoka duniani.” 34Yule towashi akamuuliza Filipo, “Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?” 35Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza habari njema za Yesu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.