Matendo 8:31
Acts 8:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.
Acts 8:31 in English
Acts 8:31 · Berean Standard Bible
“How can I,” he said, “unless someone guides me?” And he invited Philip to come up and sit with him.
Context
29Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda kwenye lile gari ukae karibu nalo.” 30Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, “Je, unaelewa hayo usomayo?” 31Yule towashi akasema, “Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye. 32Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko:
“Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni,
kama mwana-kondoo anyamazavyo
mbele yake yule amkataye manyoya,
hivyo hakufungua kinywa chake. 33Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake.
Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake?
Kwa maana maisha yake yaliondolewa
kutoka duniani.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.