Matendo 22:28
Acts 22:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo yule jemadari akasema, “Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu.” Paulo akasema “Lakini mimi ni raiya wa Rumi kwa kuzaliwa.”
Acts 22:28 in English
Acts 22:28 · Berean Standard Bible
“I paid a high price for my citizenship,” said the commander. “But I was born a citizen,” Paul replied.
Context
26Yule kiongozi aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari na kumwambia, “Unataka kufanya nini? Kwa maana huyu mtu ni raiya wa Rumi.” 27Yule jemadari akaja akamuuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raiya wa Rumi?”
Paulo akajibu, “Naam, hakika ndiyo.” 28Ndipo yule jemadari akasema, “Mimi ilinigharimu kiasi kikubwa cha fedha kupata uraia wangu.”
Paulo akasema “Lakini mimi ni raiya wa Rumi kwa kuzaliwa.” 29Mara wale waliokuwa wanataka kumhoji wakajiondoa haraka, naye yule jemadari akaingiwa na hofu alipotambua ya kuwa amemfunga Paulo, ambaye ni raia wa Rumi, kwa minyororo. 30Kesho yake, kwa kuwa yule jemadari alitaka kujua hakika kwa nini Paulo alikuwa anashutumiwa na Wayahudi, alimfungua, na akawaagiza viongozi wa makuhani na baraza lote likutane. Kisha akamleta Paulo, akamsimamisha mbele yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.