Matendo 2:16
Acts 2:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema:
Acts 2:16 in English
Acts 2:16 · Berean Standard Bible
No, this is what was spoken by the prophet Joel:
Context
14Ndipo Petro akasimama pamoja na wale mitume kumi na mmoja, akainua sauti yake na kuhutubia ule umati wa watu, akasema: “Wayahudi wenzangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, jueni jambo hili mkanisikilize. 15Hakika watu hawa hawakulewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saa tatu asubuhi! 16La, hili ni jambo lililotabiriwa na nabii Yoeli, akisema: 17“ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu,
nitamimina Roho wangu
juu ya wote wenye mwili.
Wana wenu na binti zenu watatabiri,
vijana wenu wataona maono,
na wazee wenu wataota ndoto. 18Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,
katika siku zile nitamimina Roho wangu,
nao watatabiri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.