Matendo 16:31
Acts 16:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako.”
Acts 16:31 in English
Acts 16:31 · Berean Standard Bible
They replied, “Believe in the Lord Jesus and you will be saved, you and your household.”
Context
29Yule askari wa gereza akaagiza taa ziletwe, akaingia ndani ya kile chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka mbele ya Paulo na Sila. 30Kisha akawaleta nje akisema, “Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?” 31Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka, pamoja na watu wa nyumbani mwako.” 32Wakamwambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwako nyumbani mwake. 33Wakati ule ule, yule mkuu wa gereza akawachukua, akawaosha majeraha yao, kisha akabatizwa yeye pamoja na wote waliokuwa nyumbani mwake bila kuchelewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.