Native Bible

Acts 14:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha.

Acts 14:26 in English

Acts 14:26 · Berean Standard Bible

From Attalia they sailed to Antioch, where they had been commended to the grace of God for the work they had just completed.

Context

24Kisha wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. 25Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia. 26Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha. 27Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa. 28Nao wakakaa huko pamoja na wanafunzi kwa muda mrefu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.