Matendo 14:25
Acts 14:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia.
Acts 14:25 in English
Acts 14:25 · Berean Standard Bible
And when they had spoken the word in Perga, they went down to Attalia.
Context
23Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini. 24Kisha wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. 25Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia. 26Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha. 27Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.