Native Bible

Acts 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu.

Acts 12:3 in English

Acts 12:3 · Berean Standard Bible

And seeing that this pleased the Jews, Herod proceeded to seize Peter during the Feast of Unleavened Bread.*

Context

1Wakati huo huo Mfalme Herode Agripa aliwakamata baadhi ya watu wa kanisa. 2Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. 3Alipoona jambo hilo limewapendeza Wayahudi, akaendelea, akamkamata pia Petro. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. 4Baada ya kumkamata alimtia gerezani, chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, vyenye askari wanne kila kimoja. Herode alikuwa amekusudia kumtoa na kumfanyia mashtaka mbele ya watu baada ya Pasaka. 5Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.