Matendo 12:24
Acts 12:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo.
Acts 12:24 in English
Acts 12:24 · Berean Standard Bible
But the word of God continued to spread and multiply.
Context
22Watu waliokuwa wamekusanyika wakapiga kelele, wakisema, “Hii si sauti ya mwanadamu, bali ni ya Mungu.” 23Ghafula, kwa kuwa Herode hakumpa Mungu utukufu, malaika wa Bwana akampiga, naye akaliwa na chango, akafa. 24Lakini neno la Mungu likaendelea mbele na kuenea, nao wengi wakaambatana nalo. 25Barnaba na Sauli walipomaliza ile huduma yao iliyowapeleka, wakarudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana aitwaye Marko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.