Matendo 11:3
Acts 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wakisema, “Ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.”
Acts 11:3 in English
Acts 11:3 · Berean Standard Bible
and said, “You visited uncircumcised men and ate with them.”
Context
1Mitume na ndugu walioamini waliokuwa huko Uyahudi wakasikia kuwa watu wa Mataifa nao wamepokea neno la Mungu. 2Hivyo Petro alipopanda Yerusalemu, wale wa tohara waliokuwa wameamini wakamshutumu, 3wakisema, “Ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao.” 4Ndipo Petro akaanza kuwaeleza kuhusu mambo yote yalivyotokea hatua kwa hatua akisema, 5“Nilikuwa katika mji wa Yafa nikiomba, nami nikapitiwa na usingizi wa ghafula, nikaona maono. Kulikuwa na kitu kama nguo kubwa ikishuka kutoka mbinguni, ikishushwa kwa ncha zake nne, nayo ikanikaribia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.