Matendo 10:27
Acts 10:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika.
Acts 10:27 in English
Acts 10:27 · Berean Standard Bible
As Peter talked with him, he went inside and found many people gathered together.
Context
25Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akaanguka miguuni pake kwa heshima. 26Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.” 27Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika. 28Akawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi. 29Ndiyo sababu ulipotuma niitwe nilikuja bila kupinga lolote. Basi sasa naomba unieleze kwa nini umeniita?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.