3 Yohana 1:13
3 John 1:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino.
3 John 1:13 in English
3 John 1:13 · Berean Standard Bible
I have many things to write to you, but I would prefer not to do so with pen and ink.
Context
11Rafiki mpendwa, usiige lile lililo baya bali lile lililo jema. Yeyote atendaye mema atoka kwa Mungu, bali atendaye mabaya hajamwona Mungu. 12Kila mtu ameshuhudia mema kuhusu Demetrio, vivyo hivyo hata na hiyo kweli yenyewe. Sisi pia twashuhudia mema juu yake, nanyi mwajua kwamba ushuhuda wetu ni kweli. 13Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kuandika kwa kalamu na wino. 14Badala yake, nataraji kukuona upesi, nasi tutaongea pamoja ana kwa ana. 15Amani iwe kwako. Rafiki zetu walioko hapa wanakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu walioko huko, kila mmoja kwa jina lake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.