2 Wathesalonike 3:13
2 Thessalonians 3:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema.
2 Thessalonians 3:13 in English
2 Thessalonians 3:13 · Berean Standard Bible
But as for you, brothers, do not grow weary in well-doing.
Context
11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. 12Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Yesu Kristo, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe. 13Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema. 14Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu. 15Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.