2 Samweli 5:19
2 Samuel 5:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.”
2 Samuel 5:19 in English
2 Samuel 5:19 · Berean Standard Bible
So David inquired of the LORD, “Should I go up against the Philistines? Will You deliver them into my hand?” “Go,” replied the LORD, “for I will surely deliver the Philistines into your hand.”
Context
17Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 18Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 19kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”
Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.” 20Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.* 21Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.