2 Samweli 3:32
2 Samuel 3:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakamzika Abneri huko Hebroni, naye mfalme akalia kwa sauti kwenye kaburi la Abneri. Pia watu wote wakalia.
2 Samuel 3:32 in English
2 Samuel 3:32 · Berean Standard Bible
When they buried Abner in Hebron, the king wept aloud at Abner’s tomb, and all the people wept.
Context
30(Yoabu na Abishai ndugu yake walimuua Abneri kwa sababu alikuwa amemuua Asaheli ndugu yao katika vita huko Gibeoni.) 31Kisha Daudi akamwambia Yoabu na watu wote aliokuwa pamoja nao, “Rarueni nguo zenu na mvae nguo za gunia na mtembee mkiomboleza mbele ya Abneri.” Mfalme Daudi mwenyewe akatembea nyuma ya jeneza. 32Wakamzika Abneri huko Hebroni, naye mfalme akalia kwa sauti kwenye kaburi la Abneri. Pia watu wote wakalia. 33Mfalme akaimba ombolezo hili kwa ajili ya Abneri:
“Je, ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu? 34Mikono yako haikufungwa,
miguu yako haikufungwa pingu.
Ulianguka kama yeye aangukaye
mbele ya watu waovu.”
Nao watu wote wakamlilia tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.