2 Samweli 22:9
2 Samuel 22:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake.
2 Samuel 22:9 in English
2 Samuel 22:9 · Berean Standard Bible
Smoke rose from His nostrils, and consuming fire came from His mouth; glowing coals blazed forth.
Context
7Katika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu.
Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika masikioni mwake. 8“Dunia ilitetemeka na kutikisika,
misingi ya mbingu ikatikisika,
vilitetemeka kwa sababu
alikuwa amekasirika. 9Moshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake. 10Akazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 11Alipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.