Native Bible

2 Samuel 22:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

2 Samuel 22:10 in English

2 Samuel 22:10 · Berean Standard Bible

He parted the heavens and came down with dark clouds beneath His feet.

Context

8“Dunia ilitetemeka na kutikisika, misingi ya mbingu ikatikisika, vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika. 9Moshi ukapanda kutoka puani mwake, moto uteketezao ukatoka kinywani mwake, makaa ya moto yawakayo yakatoka ndani mwake. 10Akazipasua mbingu akashuka chini, mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake. 11Alipanda juu ya kerubi akaruka, akapaa juu kwa mbawa za upepo. 12Alifanya giza hema lake la kujifunika: mawingu meusi ya mvua ya angani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.