2 Samweli 21:18
2 Samuel 21:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baada ya muda, kukawa na vita nyingine na Wafilisti, huko Gobu. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Safu, mmoja wa wazao wa Warefai.
2 Samuel 21:18 in English
2 Samuel 21:18 · Berean Standard Bible
Some time later at Gob, there was another battle with the Philistines. At that time Sibbecai the Hushathite killed Saph,* one of the descendants of Rapha.
Context
16Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai,* ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli 300 za shaba,* alikuwa amejifunga upanga mpya, naye alisema angemuua Daudi. 17Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumuua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutakwenda tena nasi vitani, ili kwamba taa ya Israeli isije ikazimwa.” 18Baada ya muda, kukawa na vita nyingine na Wafilisti, huko Gobu. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Safu, mmoja wa wazao wa Warefai. 19Katika vita vingine na Wafilisti huko Gobu, Elhanani mwana wa Yaare-Oregimu, Mbethlehemu, alimuua nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji. 20Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita kila mguu, jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.