Native Bible

2 Samuel 21:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai,* ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli 300 za shaba,* alikuwa amejifunga upanga mpya, naye alisema angemuua Daudi.

2 Samuel 21:16 in English

2 Samuel 21:16 · Berean Standard Bible

Then Ishbi-benob, a descendant of Rapha,* whose bronze spear weighed three hundred shekels * and who was bearing a new sword, resolved to kill David.

Context

14Wakazika mifupa ya Sauli na ya mwanawe Yonathani katika kaburi la Kishi, babaye Sauli, huko Sela katika nchi ya Benyamini, nao wakafanya kila kitu mfalme alichoagiza. Baada ya hayo, Mungu akajibu maombi kwa ajili ya nchi. 15Kwa mara nyingine tena kulikuwa na vita kati ya Wafilisti na Israeli. Daudi akashuka pamoja na watu wake ili kupigana dhidi ya Wafilisti, naye akawa amechoka sana. 16Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai,* ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli 300 za shaba,* alikuwa amejifunga upanga mpya, naye alisema angemuua Daudi. 17Lakini Abishai mwana wa Seruya akaja kumwokoa Daudi; akampiga huyo Mfilisti, akamwangusha chini na kumuua. Ndipo watu wakamwapia Daudi, wakisema, “Kamwe hutakwenda tena nasi vitani, ili kwamba taa ya Israeli isije ikazimwa.” 18Baada ya muda, kukawa na vita nyingine na Wafilisti, huko Gobu. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Safu, mmoja wa wazao wa Warefai.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.